Turudi kwenye msingi, π emmanuel mgogo, rose mhando,Joel lwaga,Walter chilambo,Goodluck Gozbert. nkπ
Jan 27, 2026
Mwimbaji anayesikika kwenye wimbo huu AMELINA JOHN ni wa kubuniwa (fictional) na sauti yake imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya Akili Bandia (AI).
Jina lililotumika si la mtu halisi na halimhusu mwimbaji yeyote wa kweli. Limetumika kwa madhumuni ya kisanii na kufikisha ujumbe wa kiroho tu.
Wimbo huu umetungwa kwa lengo la kuwaonya, kuwakumbusha, na kuwahimiza waimbaji wa injili na waamini wote wasipoteze mwelekeo kwa kufuata mitindo ya kidunia, tamaa ya pesa, au sifa za watu, bali warudi kwenye misingi ya mwanzo ya Injili β unyenyekevu, utakatifu, na utiifu kwa Mungu.
Picha za waimbaji wa injili zilizotumika kwenye cover au video hazilengi kumshambulia mtu binafsi wala kuhukumu mtu yeyote, bali zimetumika kama alama (mfano) kuwakilisha waimbaji wa injili kwa ujumla, ili ujumbe uwafikie kwa haraka na kwa uzito unaostahili.
Ujumbe wa wimbo huu unatukumbusha kuwa: βWakati wa hukumu umefika kuanza katika nyumba ya Mungu,β
na kwamba kila mmoja wetu anapaswa kuishi kama msafiri duniani, tukilitangaza jina la Bwana bila kuangalia mazingira au mitindo ya dunia.
Lengo si kuhukumu, bali kuonya kwa upendo, kurekebisha kwa kweli, na kuhamasisha wengi warudi kwenye njia ya haki kama kwa Muumba mwaminifu.
Tubarikiwe kwa kusikiliza, kushiriki, na kueneza ujumbe wa toba na wokovu.
ππ₯
Show More Show Less 
